
Mkutano wa saa 48 unaowakutanisha wakuu wa tawala za kijeshi nchini Mali, Niger, na Burkina Faso unafunguliwa leo Jumatatu, Desemba 22 matikamji mkuu wa Mali, Bamako.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Pamoja na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Viongozi hao watatu, walioungana ndani ya Muungano wa Mataifa ya Sahel (ESA), wanakusudia kuimarisha ushirikiano wao wa kikanda. Kulingana na mpango rasmi, Jenerali Abdourahamane Tiani, rais wa Baraza la taifa kwa ulinzi wa nchi nchini Niger, na Kapteni Ibrahim Traoré, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burkinabe, watapokelewa katika uwanja wa ndege na mwenzao wa Mali, Jenerali Assimi Goita.
“Ulinzi na usalama vitakuwa mada kuu katika ajenda ya mkutano huo,” kinabainisha chanzo rasmi cha Mali. Mjini Bamako, viongozi hao wamepangwa kukutana na uongozi wa kikosi kilichounganishwa cha ESA, ambacho kilianzishwa hivi karibuni.
Kikosi hiki, kinachoundwa na wanajeshi kutoka nchi hizo tatu, kina jukumu la kupambana na ukosefu wa usalama na makundi ya wanajihadi katika eneo la EAS. Mali, Burkina Faso, na Niger walijiondoa kutoka G5 Sahel, shirika la kikanda lililoundwa kuratibu mapambano dhidi ya ugaidi, muda fulani uliopita.
Hali nchini Benin pia kuajadiliwa
Wakati wa mkutano wao, wakuu wa nchi pia wanatarajiwa kuidhinisha utiaji saini, na mawaziri wao wa mambo ya nje, wa itifaki ya kuanzisha Televisheni ya EAS, ambayo makao yake makuu yatakuwa Bamako. Majadiliano pia yatazingatia uundaji uliopendekezwa wa benki ya pamoja ya uwekezaji, mada ambayo iliibuliwa mara kwa mara katika mikutano ya awali.
Jaribio la mapinduzi la Desemba 7 huko Cotonou pia linatarajiwa kushughulikiwa. Kwa kuwa Burkina Faso na Niger zinashiriki mpaka na Benin, “ni kawaida kabisa kwamba kuna ubadilishanaji wa taarifa kuhusu mada hii,” kinasema chanzo kutoka Niger.