L'é

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Ousmane Badiane
    • Nafasi, Digital Journalist BBC Afrique
    • Akiripoti kutoka, Dakar
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Pazia la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 limefunguliwa rasmi Jumapili hii nchini Morocco, huku jumla ya timu 24 za taifa zikiwania taji la soka la bara hili.

AFCON ni mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika, jukwaa ambalo kwa miongo kadhaa limekuwa kipimo cha maendeleo, uthabiti na ushindani wa soka la mataifa ya Afrika.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957, mataifa 44 tayari yameshawahi kushiriki angalau mara moja katika fainali za AFCON, huku vigogo wa soka kama Misri, Nigeria, Ghana na Cameroon wakitawala historia ya mashindano hayo.

Hata hivyo, licha ya ongezeko la idadi ya timu na fursa zilizopanuliwa katika miaka ya karibuni, bado kuna mataifa ambayo hayajawahi kabisa kufuzu kushiriki fainali za mashindano haya.

Kwao, ndoto ya kuingia katika jukwaa kubwa zaidi la soka barani Afrika bado ipo hai, lakini haijatimia.

Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mara nyingi hutajwa kama taifa lenye uwezo mkubwa zaidi miongoni mwa yale ambayo hayajawahi kushiriki AFCON, Jamhuri ya Afrika ya Kati sio kwamba haina vipaji bali inakumbwa na changamoto za kudumu za ukosefu wa utulivu.

Wachezaji kadhaa wa kimataifa wanacheza soka Ulaya au katika ligi za ushindani barani Afrika, lakini timu ya taifa inaendelea kukwamishwa na mazingira yasiyo na mpangilio mzuri pamoja na matatizo ya kiutawala na kimaandalizi.

Licha ya kuonyesha nyakati fulani uwezo wa hali ya juu, timu hiyo imekuwa ikishindwa mara kwa mara kufuzu AFCON.

Ikiwa katika nafasi ya 37 ya ubora barani Afrika na 128 duniani, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilimaliza mkiani mwa kundi lake katika kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco.

Djibouti

Ikiwa ni kitovu cha kijeshi na kimkakati, Djibouti haijawahi kulipa kipaumbele kikubwa soka kama ajenda ya kitaifa.

Shirikisho la Soka la Djibouti lilianzishwa mwaka 1979, likaingia CAF mwaka 1986 na FIFA mwaka 1994. Timu ya taifa ilicheza mechi yake ya kwanza kabisa mwaka 1947 dhidi ya Ethiopia.

Licha ya maboresho ya kiutawala katika miaka ya karibuni, timu ya taifa inakabiliwa na ukosefu wa ushindani wa kiwango cha juu, miundombinu duni na uzoefu mdogo wa kimataifa.

Matokeo yake, Djibouti haijawahi kufuzu AFCON wala Kombe la Dunia tangu ianze kushiriki mashindano rasmi mwaka 1998.

Eswatini

Equipe de Eswatini lors d'un match de qualification pour la CAN 2023contre le Togo en juin 2022.

Chanzo cha picha, CAF

Kwa muda mrefu ikijulikana kama Swaziland, Eswatini imekuwa ikiishi katika kivuli cha soka la Afrika Kusini.

Mafanikio yao makubwa ya hivi karibuni yalikuja kwenye kufuzu AFCON 2010 walipofika hatua ya pili kabla ya kutolewa kwenye makundi.

Katika kufuzu AFCON 2025, Eswatini ilipata sare dhidi ya Guinea-Bissau na ushindi dhidi ya Zimbabwe, ikiwa ni moja ya kampeni bora kwao katika miaka ya karibuni, lakini haikutosha kufuzu.

Kwa sasa, Eswatini iko nafasi ya 44 barani Afrika na 148 duniani kwa mujibu wa FIFA.

Lesotho

Lesotho ni taifa dogo lisilo na bandari kusini mwa Afrika, ambalo kwa miongo kadhaa limekuwa likijaribu kujijenga katika soka la bara.

Ikiwa mwanachama wa FIFA tangu 1992, timu ya taifa haijawahi kushiriki fainali za AFCON.

Changamoto kubwa ni rasilimali ndogo za kifedha, mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha na ukosefu wa mechi za kirafiki za kiwango cha juu.

Kutokuwepo kwa mpango wa maendeleo wa muda mrefu kumeathiri mwendelezo wa mafanikio.

Chad

Un joueur tchadien aux prises avec un adversaire soudanais, en éliminatoires de la Coupe du monde Qatar 2022.

Chanzo cha picha, CAF ONLINE

Chad haijawahi kushiriki fainali za AFCON wala Kombe la Dunia.

Safari zao za kufuzu mara nyingi huisha mapema, huku timu hiyo ikiwahi hata kusimamishwa kushiriki mashindano ya AFCON 2019 na 2021 kutokana na vikwazo vya CAF.

Ikiwa miongoni mwa mataifa ya mwisho katika viwango vya FIFA barani Afrika, Chad sasa inajaribu kujijenga upya chini ya makocha kadhaa akiwemo Mswisi Raoul Savoy.

Somalia

Migogoro ya muda mrefu ya kisiasa imezuia maendeleo ya michezo nchini Somalia.

Timu ya taifa, Ocean Stars, haijacheza mechi ya nyumbani ya kimataifa tangu mwaka 1986.

Kwa sasa Somalia iko nafasi ya 200 duniani, ikiwa bado inahangaika kujenga msingi wa ushindani wa soka la kimataifa.

Sao Tomé na Principe

Taifa hili dogo la visiwa linakabiliwa na changamoto za kijiografia na kiuchumi.

Kwa idadi ya watu wasiopungua 220,000, wigo wa vipaji ni mdogo sana, huku ligi ya ndani ikiwa ya kiwango cha ridhaa.

Licha ya rasilimali haba, Sao Tome inaendelea kushiriki mashindano ya CAF na FIFA, lakini kufuzu AFCON bado ni ndoto ya mbali.

Sudan Kusini

Equipe nationale du Soudan du Sud

Chanzo cha picha, Fédération Sud-Soudanaise de Football

Ikiwa taifa changa zaidi duniani, Sudan Kusini bado inajenga soka lake kutoka kwenye msingi.

Licha ya changamoto za miundombinu, fedha na siasa, timu ya taifa imekuwa chombo cha umoja wa kitaifa.

Ikiwa nafasi ya 47 barani Afrika na 169 duniani, Sudan Kusini bado inapigania kujijenga katika ngazi ya ushindani wa bara.

Seychelles

Uchumi wa Seychelles umejikita zaidi kwenye utalii, huku michezo ya ushindani ikibaki nyuma katika vipaumbele vya kitaifa.

Tofauti ya kiwango kati yao na mataifa makubwa ya Afrika ni kubwa.

Seychelles haijawahi kufuzu fainali za AFCON, na mara nyingi humaliza mkiani mwa makundi ya kufuzu, ikikumbana na vipigo vizito.

Eritrea

Les

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Kwa hali ya kipekee barani Afrika, Eritrea imekuwa karibu kutokuwepo kabisa katika soka la kimataifa kwa miaka ya karibuni.

Kujiondoa kwenye mashindano, kususia mechi na mazingira ya kisiasa yameathiri moja kwa moja maendeleo ya soka.

Nchi hiyo haipo tena kwenye viwango vya FIFA, kutokana na kutoshiriki mechi rasmi kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *