ol

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Wakati tukielekea mwisho mwa mwaka 2025, tudurusu vifo vya watu mashuhuri katika mwaka huu, ambao walikuwa maarufu katika kazi zao, kuanzia dini hadi michezo.

Pia unaweza kusoma

Dini

ik

Chanzo cha picha, Reuters

Papa Francis, 88

Papa wa kwanza kutoka Amerika Kusini, Papa Francis alifariki dunia Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88, nyumbani kwake katika Jiji la Vatican, baada ya kuugua kwa muda mrefu, kutokana na kiharusi cha ubongo.

Zaidi ya watu 250,000 walihudhuria mazishi yake mwezi Aprili, kulingana na Vatican.

Aga Khan, 88

Karim Al Husseini, Aga Khan wa nne, alifariki mwezi Februari. Mfanyabiashara tajiri na kiongozi wa kiroho wa wa Waislamu milioni 15 wa madhehebu ya Ismailia.

Sayansi

o

Chanzo cha picha, Reuters

Jane Goodall, 91

Mwanaharakati wa kimataifa, ambaye alikuwa na mapenzi makubwa kwa nyani na kuwa sehemu ya maisha yake ya kulinda mazingira, alifariki mwezi Oktoba.

Jim Lovell, 97

Kamanda wa Apollo 13, wa safari ya NASA ya mwaka 1970 iliyoshindwa kwenda Mwezini ambayo inaelezwa katika filamu iliyoigizwa na Tom Hanks.

James Watson, 97

Mwanabiolojia ambaye ugunduzi wake wa muundo wa DNA ulianzisha enzi juu ya vinasaba.

Michezo

o

Chanzo cha picha, Reuters

George Foreman, 76

Bingwa wa ndondi za uzito wa juu alipoteza taji lake la kwanza kwa Muhammad Ali katika pambano lao maarufu la 1974 huko Kinshasa – “The Rumble in the Jungle.”

Hulk Hogan, 71

Alikuwa sura ya mieleka katika miaka ya 1980, akisaidia kubadilisha mchezo huo kutoka kuwa wa kutisha hadi kuwa burudani rafiki kwa familia – na kupanda thamani ya mabilioni ya dola. Alifariki Julai.

Diogo Jota, 28

Mchezaji huyo wa soka wa Ureno alifariki mwezi Julai wakati gari aina ya Lamborghini alilokuwa nalo lilipotoka barabarani na kuwaka moto. Wiki chache nyuma, alitoka kubeba kombe la Ligi Kuu kwa Liverpool.

Fasihi

k

Chanzo cha picha, Reuters

Ngũgĩ wa Thiong’o, 87

Mwandishi wa Kenya ambaye ukosoaji wake dhidi ya serikali baada ya uhuru ulisababisha kufungwa na kupelekwa uhamishoni.

Mario Vargas Llosa, 89

Mwandishi wa Peru, ambaye ni mwangaza katika hadithi za kubuni za Amerika Kusini, alishinda Tuzo ya Nobel ya fasihi mwaka 2010. Alifariki mwezi Aprili.

Siasa

s

Chanzo cha picha, Reuters

Dick Cheney, 84

Mmoja wa makamu wa rais mwenye nguvu zaidi katika historia ya Marekani, Cheney alikuwa kichocheo cha uvamizi wa Iraq mwaka 2003. Alifariki mwezi Novemba.

Charlie Kirk, 31

Mwanaharakati wa siasa za kihafidhina alipewa sifa ya kujenga ngome ya Donald Trump miongoni mwa wapiga kura vijana. Aliuawa hadharani Septemba.

Jean-Marie Le Pen, 96

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa alifariki mwezi Januari.

Mwaka 2015, binti yake na mrithi wake Marine Le Pen walimfukuza katika chama kwa kusema tena kwamba vyumba vya gesi vya Nazi sio jambo kubwa katika historia ya Vita vya Pili vya Dunia.

Muhammadu Buhari, 82

Akiwa rais wa Nigeria, Buhari aliongoza nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika kuanzia mwaka 2015 hadi 2023. Muda wake madarakani uliathiriwa na mdororo wa uchumi wa Nigeria, mashambulizi ya wanamgambo kwenye visima vya mafuta, na kukaa hospitalini mara kwa mara kwa ugonjwa ambao haujafichuliwa

Raila Odinga, 80

Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Kenya aligombea urais mara tano bila mafanikio. Mkanyagano katika mazishi yake mwezi Oktoba uliua watu wawili na kuwajeruhi zaidi ya wengine 160, kundi la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka lilisema.

Sam Nujoma, 95

Kiongozi huyo wa msituni alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Namibia baada ya kupata uhuru kutoka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Jose Mujica, 89

Akiwa rais wa Uruguay, aliendesha gari aina ya VW Beetle lilolochoka na alikuwa na shamba dogo la maua, akibatizwa jina la rasi masikini duniani. Mageuzi yake ya kimaendeleo yalileta sifa Amerika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *