Photo-montage avec des images de Wilglory Tanjong, Claudia Sengor, Vanessa Nakate et Mamadou Diakahaté.

Chanzo cha picha, BBC / COURTESY

    • Author, Ousmane Badiane
    • Nafasi, Digital Journalist BBC Afrique
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Mwaka 2025 ulishuhudia kuibuka kwa wimbi la kipekee la vipaji vya vijana wa kiafrika waliotikisa anga za kitaifa na kimataifa.

Kizazi kipya cha Waafrika vijana kimejitokeza kama nguvu muhimu katika ubunifu, ushawishi na mageuzi ya kijamii. Iwe ni katika uongozi wa kisiasa, ushiriki wa kiraia, kilimo-biashara, afya, utamaduni au teknolojia, vijana hawa wanaonesha bara linalosonga mbele, ambako mawazo mapya yanageuka kuwa suluhisho halisi.

BBC Africa inawakumbuka baadhi ya vijana waliotoa mchango chanya na kuacha alama kubwa mwaka huu.

Wilglory Tanjong (Cameroun)

Wilglory Tanjong, entrepreneure camerounaise basée aux États-Unis.

Chanzo cha picha, @wilgloryy via Instagram

Wilglory Tanjong ni mjasiriamali wa Cameroon anayeishi Marekani. Akiwa na umri wa miaka 28 pekee, anawakilisha kizazi kipya cha wabunifu wa Kiafrika wanaobadili taswira ya vitu vya kifahari kimataifa.

Alizaliwa Cameroon na mwaka 2020 alianzisha chapa yake ya Anima Iris, kampuni ya bidhaa za ngozi inayofanya vizuri kwenye sanaa, mitindo na urithi wa Kiafrika. Leo, mikoba yake ya kisanaa inatambulika kimataifa.

Safari ya Anima Iris ilianza kama mradi mdogo uliogharimiwa na dola 5,000 za akiba binafsi. Leo, chapa hiyo inavaliwa na watu mashuhuri, inauzwa na wauzaji wakubwa na kupongezwa na vyombo vya habari vya dunia.

Hatua kubwa ilikuja pale mwanamuziki Beyoncé alipoonekana kwa mara ya kwanza akiwa amebeba mkoba wa Anima Iris, tukio ambalo Wilglory hulielezea kama “lisiloaminika”. Mwaka 2024, Beyoncé alirudia kuvaa bidhaa hiyo, kuthibitisha ukuaji wa kasi wa chapa hiyo.

Hadi 2025, kampuni hiyo ilikuwa imeingiza zaidi ya dola milioni 2.3 ndani ya miaka minne.

Claudia Senghor (Senegal)

Claudia Senghor s'exprime lors du forum sur les systèmes alimentaires.

Chanzo cha picha, LINKEDIN

Claudia Senghor ni mhitimu wa uchumi wa kilimo na maendeleo endelevu kutoka Chuo Kikuu cha Laval nchini Canada. Mwaka 2021 alianzisha Agrobabe, jukwaa linalotoa mafunzo, ushauri na maudhui kuhusu ujasiriamali wa kilimo.

Kwa jamii ya zaidi ya wafuasi 350,000, Claudia amebadilisha mtazamo wa vijana kuhusu kilimo kwa kuunganisha taaluma, elimu rahisi kueleweka na mvuto wa kisasa.

Mwaka 2025, alialikwa kama mchangiaji mkuu katika Jukwaa la mifumo ya chakula barani Afrika (AFSA), ambako alitambuliwa kama mmoja wa vijana wanaochangia mustakabali wa chakula barani Afrika.

Mamadou Diakhaté (Senegal)

Mamadou Diakhate creuse des puits dans les villages sénégalais confrontés à la pénurie d'eau, grâce au crowdfunding sur les médias sociaux.

Mamadou Diakhaté ambaye ni mwalimu kwa taaluma, amejitolea maisha yake kusaidia jamii zilizo pembezoni. Kupitia michango ya mitandaoni na timu yake ya kujitolea, amechimba zaidi ya visima 100 katika vijiji vinavyokumbwa na tatizo la uhaba wa maji.

Kupitia shirika lake linaloitwa Simple Action Citoyenne, pia anasambaza vifaa vya shule na kukarabati shule chakavu.

Mwaka 2025, alizindua mradi mkubwa mjini Dakar uitwao The Dakar Epic, unaolenga kutoa fursa za mafunzo, ujasiriamali na ushauri kwa vijana wapatao 6,000 kila mwaka.

Stephane Kulimushi Mutanda (RDC)

Stéphane Kulimushi Mutanda, réfugié de la République démocratique du Congo installé désormais en Ouganda.

Chanzo cha picha, ONU INFOS

Stéphane Kulimushi Mutanda ni mjasiriamali na mchezaji wa mpira wa kikapu, ambaye ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi Uganda.

Akiwa na umri wa miaka 19, alianzisha Refugee Basketball Academy, mpango unaotumia michezo kuwawezesha vijana wakimbizi kupitia elimu na uongozi.

Mwaka 2025, aliteuliwa na Umoja wa Mataifa kama mmoja wa vijana 17 waliotambuliwa kutoa michango kwenye malengo ya maendeleo endelevu duniani (Young Leaders for the SDGs).

Vanessa Nakate (Ouganda)

Vanessa Nakate s'exprime à la tribune des Nations Unies

Chanzo cha picha, ONU INFO

Vanessa Nakate ni mwanaharakati wa kwanza kutoka Uganda katika harakati za Fridays for Future. Ni Balozi wa UNICEF na mwanzilishi wa miradi kadhaa ya mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo Vash Green Schools, inayosambaza nishati ya jua mashuleni.

Mwaka 2025, alijiunga na Project Dandelion, kampeni ya kwanza ya kimataifa inayoongozwa na wanawake kwa ajili ya haki ya tabianchi.

Hafsat “Havfy” Abdullahi (Nigéria)

Hafsat (Havfy) Abdullahi, Nigeria.

Chanzo cha picha, ONU INFOS

Hafsat Abdullahi ni mshairi na mwanaharakati wa kijamii kutoka kaskazini mwa Nigeria. Kupitia mashairi yake, anajadili masuala nyeti ya kijamii na kuwahamasisha vijana.

Ametambuliwa na taasisi kubwa kama Benki ya Dunia, UNICEF na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ni miongoni mwa viongozi vijana wa Umoja wa Mataifa 2025.

Betelhem Dessie (Ethiopie)

Betelhem Dessie, téléphone à l'oreille, est assise devant son PC, le drapeau américain en arrière plan.

Chanzo cha picha, Courtesy of Betelhem Dessie

Betelhem Dessie ni mmoja wa nyuso zinazoibuka kwa kasi katika teknolojia barani Afrika. Alianza kufanya kazi ya kutengeneza programu mbalimbali za kompyuta akiwa na umri wa miaka 10.

Ni mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa iCog Anyone Can Code, shirika lililowafundisha zaidi ya vijana 26,000 ujuzi wa programu, roboti na akili bandia.

Jacques Kwibuka (Rwanda)

Jacques Kwibuka, Rwanda.

Chanzo cha picha, ONU INFOS

Jacques Kwibuka ni mwanzilishi wa Informed Future Generations, jukwaa linalowawezesha vijana kushiriki katika afya, elimu na sera za umma.

Kazi yake inalenga afya ya uzazi, virusi vya Ukimwi (VVU), afya ya akili na uongozi wa vijana. Mwaka 2025, aliteuliwa pia kuwa mmoja wa Viongozi Vijana wa Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *