Chombo cha habari cha Arabi21 kimeripoti kuwa, ingawa jeshi la Israel limezuia kuingia bidhaa nyingi muhimu huko Gaza, ripoti zinaonyesha kuwa usafirishaji haramu wa dawa za kulevya katika eneo hilo unarahisishwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, shughuli hizi zinafanywa kupitia mtandao wa mawakala wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanaofanya kazi ndani na nje ya Gaza.

Madawa hayo ya kulevya yanafichwa ndani ya bidhaa za kiraia na shehena za kibiashara.

Kivuko cha Kissufim kimetambuliwa kama mojawapo ya njia kuu za magendo ya dawa hizo.

Vyanzo vya usalama vinasisitiza kwamba lengo la vitendo hivi ni kuwadhuru vijana wa Gaza na kueneza uraibu wa dawa za kulevya ndani ya jamii.

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ya Gaza imekamata kiasi kikubwa cha hashishi na ecstasy, ikielezea jambo hilo kama “vita vya kimya kimya” vinavyoendeshwa dhidi ya mfumo wa kijamii wa Ukanda wa Gaza.

Ecstasy ni dawa ya kupevya inayoathiri kemia ya ubongo kwa kutoa kiwango cha juu cha serotonini, ambayo ina jukumu katika kudhibiti hisia, kiwango cha nishati na hamu ya kula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *