Wizara ya Afya ya Gaza imetahadharisha kuhusu uhaba mkubwa na hatari zaidi wa dawa na vifaa vya matibabu. Imesema kuwa uhaba huo umelemaza uwezo wa eneo hilo wa kutoa huduma ya dharura ya matibabu na kuokoa maisha ya wagonjwa kufuatia kuendelea mzingiro wa Israel dhidi ya Gaza.

Wizara ya Afya ya Gaza imeeleza kuwa dawa muhimu 321 zimemalizika kabisa, kiwango ambacho ni sawa na ukosefu wa dawa wa asilimia 52.  

 Hii ni katika hali ambayo vipimo vya maabara na vifaa vya benki ya damu pia vimepungua sana na kiwango cha uhaba ni cha asilimia 59.

Wizara ya Afya ya Gaza pia imetahadharisha kuwa ukosefu wa vifaa tiba utasababisha kukosa huduma ya dharura karibu wagonjwa 200,000, wagonjwa 100,000 kukosa huduma za upasuaji na takriban wagonjwa 700 huduma nyingine kubwa za kitiba. 

Wizara hiyo imetoa wito kwa pande zote husika kutekeleza haraka iwezekanavyo majukumu yao ili kukidhi mahitaji hayo ya dharura ya matibabu.

Wakati huo huo, madaktari katika Ukanda wa Gaza wanaendelea kutatizika katika jitihada za kuokosa maisha ya wagonjwa kutokana na Israel kuendelea kuzuia kuingizwa vifaa muhimu vya matibabu katika eneo hilo. 

Karibu hospitali na zahanati zote za Ukanda wa Gaza zilishambuliwa katika vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni; ambapo vituo vya matibabu visivyopungua 123 vimeharibiwa zikiwemo hospitali 34. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *