
Msemaji rasmi wa Kamati ya Uchunguzi Svetlana Patrenko amesema mapema leo kwamba Jenereli Sarvarov amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata na kuongeza kuwa tayari wameanzisha uchunguzi.
Amesema “Wachunguzi wanafuatilia sababu mbalimbali kuhusiana na mauaji hayo. na moja ya sababu hizo ni uhusika wa idara ya Ujasusi ya Ukraine.”
Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kwamba gari hilo lililipuka majira ya saa moja asubuhi, likiwa kwenye maegesho ya magari katika mtaa wa Yaseneva mjini Moscow, na dereva akiwa ndani ya gari.
Idara za usalama za Ukraine zilidai kufanya shambulizi kama hili dhidi ya mkuu wa vikosi vya ulinzi wa nyuklia, baiolojia na kemikali vya Urusi Disemba 2024 Luteni Kanali Igor Kirillov, aliyeuawa kwa bomu lililotegwa kwenye pikipiki nje ya makazi yake.