Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Sihasak Phuangketkeow amewaambia waandishi wa habari mjini Kuala Lumpur kwamba majadiliano hayo yatafanyika katika mfumo wa kamati iliyopo ya pamoja ya mipaka ya JBC.

Ameongeza kuwa tayari mkutano umepangwa kufanyika Disemba 24, kufuatia pendekezo laCambodia

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya ushirikiano ya Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN walikutana mapema leo nchini Malaysia kujaribu kuurejesha mpango wa usitishaji mapigano kati ya mataifa hayo jirani, baada ya wiki mbili za mapigano makali yaliyowaua watu wasiopungua 60 na wengine nusu milioni kuyakimbia makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *