
China aidha imesema inapinga vikwazo vyote vya upande mmoja na vinavyotolewa kinyume cha sheria.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian ameongeza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba Venezuela ina haki ya kuunda ushirikiano na mataifa mengine.
Mapema Marekani ilitangaza kuwa inaifuatilia kwa lengo la kuimata meli nyingine ya mafuta inayodai kutumiwa na serikali ya Venezuela kukwepa vikwazo vya biashara ya mafuta vilivyowekwa na Washington.
Ikiwa wataikamata, itakuwa ni meli ya tatu yenye mafungamano na biashara ya mafuta ya Venezuela — taifa ambalo Marekani inalituhumu kwa kufadhili biashara ya dawa za kulevya.