
Watu walijifungia ndani kwa ajili ya usalama wao na shughuli kwenye mji huo zilisimama, hii ikiwa ni kulingana na mkaazi mmoja alipozungumza kwa simu na shirika la habari la AFP.
Mapigano yalijikita kwenye maeneo ya milimani na vitongoji vilivyopo karibu na kusini na magharibi mwa mji huo, ikiwa ni pamoja na sehemu ya Kalundu, ulioko Mto Tanganyika, wakazi wamesema.
Kiongozi wa tawi la kisiasa la M23, Corneille Nangaa alitangaza kwamba kundi hilo “lingewaondoa wapiganaji wote kwenye mji wa Uvira ilioudhibiti, kama walivyoombwa na wapatanishi wa Marekani, ingawa inaarifiwa bado wangalipo, wakiwa wamevalia nguo za kiraia.