BEI ya dhahabu imepanda na kuvunja rekodi, ikiuza kwa zaidi ya dola 4,400 kwa gramu kwa mara ya kwanza katika historia ya soko hilo. Wachambuzi wa masoko wanasema ongezeko hilo linatokana na matarajio kwamba Benki Kuu ya Marekani (Fed) itapunguza viwango vya riba mwaka ujao, hali inayoongeza mvuto wa dhahabu kama mali salama kwa wawekezaji.
Mwanzoni mwa mwaka huu, dhahabu ilikuwa ikiuzwa kwa takribani dola 2,600 kwa gramu. Hata hivyo, mivutano ya kisiasa na kijiografia duniani, pamoja na sera za ushuru zilizowekwa na Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, vimeongeza mahitaji ya dhahabu na mali nyingine salama. SOMA: Mara yachimba dhahabu ya Trilioni 8.8/-
Sambamba na hilo, bei za madini mengine ya thamani kama fedha na platinamu nazo zimeendelea kupanda katika masoko ya kimataifa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti katika soko la dhahabu la BullionVault, Adrian Ash, bei ya dhahabu imepanda kwa zaidi ya asilimia 68 mwaka huu, ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 1979.
