
MAMLAKA ya Kulinda Mazingira nchini Ethiopia imetangaza kuwa itaanza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari 31, 2026. Hatua hiyo inafuatia tangazo lililothibitishwa na Bunge mwezi Julai 2025.
Tangu kupitishwa kwa sheria hiyo, mamlaka imekuwa ikihamasisha wazalishaji na umma kuhusu athari za mifuko ya plastiki kwa mazingira. Chini ya kanuni mpya, itakuwa ni kinyume cha sheria kutumia, kuzalisha, au kuagiza nje mifuko ya plastiki.
Mamlaka imesisitiza kuwa marufuku hiyo ni hatua muhimu ya kupunguza uchafuzi wa mazingira na kulinda mazingira ya Ethiopia kwa vizazi vijavyo. SOMA: Mpango aitaka NEMC kusimamia katazo la mifuko ya plastiki