Zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika katika mradi wa kuimarisha mbinu za asili za usimamizi wa maji na kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika Bonde la Usangu, mradi wa miaka mitatu unaoratibiwa na Bonde la Rufiji.

Mradi huo unalenga kurejesha mito kwenye njia za asili, kuhifadhi kingo za mito na vyanzo vya maji, kuchimba visima vya kunywa kwa jamii, pamoja na kujenga mabirika kwa ajili ya mifugo ili kupunguza uharibifu wa kingo za mito na kuhakikisha maji yanapatikana kwa muda mrefu.

Mratibu wa mradi huo, David Mginya amesema hatua hizo zitaleta manufaa kwa jamii za Bonde la Usangu na kuongeza upatikanaji wa maji safi kwa watu na mifugo.

✍ Kakuru Msimu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *