Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amefika katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Amani Makolo–Ruanda wilayani Mbinga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, kufuatia malalamiko ya wananchi dhidi ya mkandarasi wa mradi huo.
Wananchi wamelalamikia kusuasua kwa ujenzi, wakidai mkandarasi ameacha kazi ya barabara na kujikita kwenye biashara ya kokoto, hali inayosababisha adha kubwa kwao.
Mbele ya viongozi hao, wananchi wamemuomba Waziri Ulega kuchukua hatua kali ikiwemo kumuondoa mkandarasi, wakisisitiza kuwa ucheleweshaji huo umeathiri maisha na shughuli zao za kila siku.
Mawazo Mwaijengo
Mhariri | @claud_jm
#UTV108 #AzamTVUpdates #AdhuhuriLive