Mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa RSF na jeshi la taifa la Sudan sasa yanajikita jimboni Kordofan ambako jeshi la Sudan linadhibiti miji kadhaa iliyozingirwa na wapiganaji wa RSF. Kordofan pia ni eneo la mwisho linalotenganisha maeneo yanayoshikiliwa na jeshi kaskazini na katikati, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Sudan Khartoum, na maeneo yanayodhibitiwa na RSF huko Darfur magharibi mwa Sudan pamoja na sehemu za kusini.

Jan Sebastian Friedrich-Rust, mkurugenzi mtendaji wa tawi la Ujerumani la Shirika lisilo la kiserikali la kukabiliana na njaa la “Action against Hunger”, amethibitisha kuwa vurugu huko Kordofan zimeongezeka mno katika siku za hivi karibuni huku kukiripotiwa vitendo kadhaa vya ukatili dhidi ya raia.

Philippe Dam, Mkurugenzi wa mipango wa Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binaadamu la Human Rights Watch katika taasisi ya Umoja wa UIaya ametoa wito kwa pande zote katika mzozo huu wa Sudan kuwajibishwa.

Suluhisho la mzozo wa Sudan liko wapi?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

“Ukweli ni kwamba pande zote mbili katika mgogoro huo na washirika wao si tu wameshindwa kuwalinda raia, bali raia ndio wamekuwa wakilengwa zaidi katika vita hivyo. Kuna haja kubwa kwa jumuiya ya kimataifa kuitilia maanani hali inayoendelea nchini Sudan na kushughulikia uhalifu unaoendelea kufanywa. Ukatili wa kijinsia umekuwa ukitekelezwa mno katika mgogoro huu wa Sudan, wahanga wakiwa ni wanawake na wasichana wanaofanyiwa madhila hayo na wapiganaji wa pande zote mbili za mgogoro huo.”

Vita vya Sudan, mzozo unaopuuzwa

Kulingana na utafiti uliofanywa na karibu mashirika 22 ya misaada ya kimataifa na uliotolewa wiki iliyopita, vita vya Sudan ndio mgogoro wa kimataifa uliopuuzwa zaidi mnamo mwaka huu wa 2025. Nchi hiyo iliyokumbwa na vita pia ilishika nafasi ya kwanza katika “migogoro 10 ambayo dunia haiwezi kuipuuza mnamo mwaka ujao wa 2026, hii ikiwa ni kulingana na Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji.

Katika mwaka mzima wa 2025, hali katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika imezidi kuwa mbaya kutokana na vita vinavyoendelea na vilivyoanza Aprili mwaka 2023 kati ya majenerali wawili hasimu kutoka jeshi la taifa na kikosi cha RSF, ambao walitofautiana kuhusu suala la ujumuishaji wa vikosi vyenye silaha katika jeshi la taifa.

Sudan Al-Faschir 2025 | Wanamgambo wa RSF
Mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa RSF na jeshi la taifa la Sudan sasa yanajikita jimboni KordofanPicha: Rapid Support Forces (RSF)/AFP

Tangu wakati huo, Sudan yenye utajiri wa mafuta na dhahabu, pamoja na ardhi yake kubwa ya kilimo, imegeuka kuwa kile kilichotajwa na  Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada kuwa mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu kutokana na idadi kubwa ya watu kulazimika kuyahama makazi yao. Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni 14 wamekuwa wakimbizi wa ndani na wengine kadhaa wakikimbilia katika nchi jirani.

Idadi ya vifo inakadiriwa kuwa kati ya watu 40,000 na 250,000. Takwimu sahihi au zilizotolewa hivi karibuni hazipatikani kutokana na kwamba mapigano yanaendelea, bado kuna matatizo ya mawasiliano ya intaneti inayotumia satelaiti huku mashirika mengi ya misaada na waangalizi wa kimataifa wakiwa wameondoka nchini humo.

Mkurugenzi anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu katika shirika la kuwasaidia watoto la ” Save the Children” Abdurahman Sharif amesema kuwa mgogoro wa Sudan ungelipaswa kugonga vichwa vya habari kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *