Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 2
Manchester United wanataka kumsajili kiungo mpya Januari na wamemuweka kwenye orodha yao Conor Gallagher wa Atletico Madrid, wakimtaka kwa mkopo wakiamini ni rahisi kumpata.
Tottenham wamejiondoa kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji Antoine Semenyo wa Bournemouth, lakini bado yupo kwenye rada za Manchester City na Manchester United, huku Liverpool wakifuatilia hali hiyo kutokana na jeraha la Alexander Isak.
Semenyo ana kipengele cha kuvunjwa mkataba chenye thamani ya pauni milioni 60.5, na inaripotiwa kuwa tayari amefanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.
Aston Villa wameanza mawasiliano na wawakilishi wa Brennan Johnson wa Tottenham, ambaye hapati nafasi ya mara kwa mara, huku Crystal Palace nao wakionyesha nia.
Chelsea wako tayari kumruhusu beki Axel Disasi ajiunge na AC Milan Januari, lakini klabu hiyo ya Italia bado inafanya tathmini ya machaguo yake kabla ya kuchukua hatua.
Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea na Manchester City wanamfuatilia winga chipukizi wa England Jeremy Monga mwenye umri wa miaka 16 kutoka Leicester, na huenda wakajaribu kumsajili Januari.
Roma wametoa ofa ya awali ya euro milioni 5 kwa ajili ya kumsajili Joshua Zirkzee wa Manchester United kwa mkopo Januari, na euro milioni 30 zaidi ili kumnunua moja kwa moja mwezi Juni.
Newcastle United wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji William Osula kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja baadaye. Mchezaji huyo anapendelea kujiunga na klabu ya Ujerumani na anasubiri makubaliano yakamilike.
Manchester United na Newcastle United pia wanamfuatilia kiungo wa Ureno Ruben Neves, huku klabu yake ya sasa ikiwa tayari kumuachia Januari.
Mshambuliaji kinda wa Real Madrid, Endrick, anatarajiwa kujiunga na Lyon kwa mkopo wa miezi sita.
Bayer Leverkusen wanachunguza uwezekano wa kumsajili winga kijana wa Brighton Harry Howell, huku vilabu vingine vya Ujerumani navyo vikiwa na nia ya kumsajili.
Chelsea wamemtaja kiungo wa Lille mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi, kama lengo lao kuu la usajili dirisha la Januari.