Zelensky alikuwa akizungumza na mabalozi mjini Kyiv ambapo ametahadharisha kuwa hali itakuwa mbaya kwa sababu nchi yake haina mifumo ya kutosha ya ulinzi wa anga.

Zelensky ameelezea wasiwasi huo katika wakati Marekani na washirika wa Ukraine barani Ulaya wameongeza kasi ya diplomasia ili kutafuta mkataba wa kumaliza vita.

Ukraine ilibadili kalenda yake ya sikuuu baada ya kuzuka vita na kuanza kusherehekea Krismasi kila Disemba 25 kama ilivyo kwa utamaduni wa nchi za magharibi.

Hata hivyo, raia wengi wa taifa hilo bado wanaadhimisha sikukuu hiyo kwa kufuata desturi za madhehebu ya Wakristo wa Orthodox wanaosherehekea Krismasi kila Januari 7, kama ilivyo pia nchini Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *