Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo itakuwa na miadi na Benin itakapotimu 13:30, saa za Morocco.

Baadaye jioni, Taifa Stars ya Tanzania itaitunishia misuli Nigeria kwa mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu kwa Stars ambayo imekuwa na historia isiyoridhisha kwenye michuano ya AFCON.

Uganda-the Cranes, wenyewe wanajipanga kwa mtanange na Tunisia itakapotimu saa tatu usiku. Michezo mitatu inasubiriwa kwa shauku kubwa na mashibiki.

Katika michezo mitatu ya jana, Mali iliyo kundi A ililazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wake na Zambia.

Bafana Bafana ya Afrika Kusini iliondoka na alama tatu kwa kuichapa Angola mabao 2-1. Matokeo sawa na hayo yalipatikana pia na Mafarao wa Misri walioilaza Zimbabwe bao 2-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *