Familia na wadau mbalimbali wamefanya ibada ya kumkumbuka mwanahabari mkongwe nchini Kenya, ambaye pia ni baba mzazi wa @babbiekabae, Sammy Lui Wang’ondu ambaye alifariki October 23, 2025 katika makazi yake Subukia, Nakuru.

Tukio hilo la kumuenzi lilifanyika katika katika kanisa la All Saints Cathedral ambapo wahudhuriaji walipata nafasi ya kumuenzi na kutoa pole kwa familia.

Wakati wa uhai wake Sammy Lui amewahi kuwa mtangazaji wa vituo vya televisheni vya KBC na KTN, pia akiwa muongoza shughuli katika matukio ya ikulu ya Kenya wakati wa utawala wa Daniel Arap Moi na Mwai Kibaki.

Clouds Media inatoa pole kwa @babbiekabae na familia nzima kwa msiba huu mkubwa.

Video kwa hisani ya @citizentvkenya #TutaonanaBaadae

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *