Watumishi wa idara mbalimbali katika kata ya Nyamazugo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuchochea maendeleo ya wananchi hususani katika sekta za kilimo ,ufugaji na uvuvi katika kata hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Nyamzugo Fidel Martine katika kikao cha kwanza cha Maendeleo ya kata kilichofanyika katika kata hiyo .

Katika hatua nyingine amewakumbusha watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia utawala bora ikiwa ni pamoja na kutowaonea wananachi .

Kwa upande wao baadhi ya wananachi wamempongeza Diwani huyo kwa dira na muelekeo wake wa utendaji kazi na kwamba wanamatumaini kata hiyo itapiga hatua kubwa kimaendeleo katika utawala wake .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *