
Urusi imeishambulia miundombinu ya nishati katika mji waUkraine wa Kyiv mapema leo Jumanne, na kusababisha kukatika kwa umeme. Wizara ya nishati ya Ukraine imeongeza kwamba athari za mashambulizi hayo zimeshuhudiwa pia katika maeneo mengine kadhaa yanayouzunguka mji huo.
Mashambulizi hayo ya Urusi nchini Ukraine yameifanya nchi jirani,Poland, ambayo ni mwanachama wa NATO kukimbilia kuilinda anga yake.
Ukraine na Urusi zimeendelea kushambuliana hata baada ya mazungumzo ya amani yaMiamiyanayoongozwa na Marekani kumalizika siku mbili zilizopita.
Katika hatua nyingine, Rais Volodymyr Zelensky amesema anategemea Urusi itafanya mashambulizi makali ndani ya Ukraine wakati wa sherehe za sikukuu ya Krismasi akiutuhumu utawala mjini Moscow kwa kuonesha tabia hiyo ndani ya miaka minne ya vita.