Mbeya. Mbunge wa Uyole Dk , Tulia Ackson amevunja ukimya na kutaja sababu ya kutumia vyombo vya habari na mitandao kijamii kutangaza pindi anapotoa misaada kwa wahitaji lengo ni kuikumbusha jamii kugusa makundi hayo.
Dk.Tulia ametoa kauli hiyo Disemba 22,2025, wakati akitoa mahitaji ya chakula na fedha kwa wahitaji wakiwepo wazee wasio jiweza jimboni kwake.
Kauli ya Dk Tulia imekuja kufuatia baadhi ya watu kudai anapotoa msaada kuwatangaza walengwa kwa kutumia vyombo vya habari ikiwepo mitandao ya kijamii.
“Sisi tumenza kwa kutoa Mchele kilo 20 kwa wahitaji na wewe pia unaweza kutoa chochote ulicho jaliwa usikubali kuona wahitaji wakilala njaa wakati Mungu amekufanikisha,”amesema.
Wakati huo huo Dk Tulia ametaja hatua inayo fuata baada ya kutoa mahitaji kwa wazee ni kushona sare za wanafunzi waishio mazingira magumu kwa lengo la kurejesha tabasamu na kusoma kwa bidii.
“Ifikapo mwaka mpya tunaelekeza nguvu kwenye sekta ya elimu kwa kushona sare za wanafunzi na mahitaji mengine kama madaftari na bima za afya bure, “amesema.
Mmoja wa wanufaika hao Mzee Asyeke Chaula (80), mkazi wa Mtaa wa Itezi Mlimani ameshukuru na msaada huo na kuomba wadau wengine kuunga mkono.
“Huyu ni Mbunge wa kipee licha ya kuwa na familia yake ,lakini kawekeza nguvu kwa wananchi mpango ambao ameanza miaka kadhaa iliyopita, “amesema.