Madaktari bingwa nchini wameanzisha kambi ya siku mbili ya huduma za matibabu katika Hospitali ya Direct Aid, Tabata, Dar es Salaam, ikiwa na lengo la kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali na kubaini changamoto za magonjwa ya ndani ikiwemo kisukari, presha, na vidonda vya tumbo.

Akizungumza na Azam News, Mkurugenzi wa Hospitali ya Direct Aid na daktari bingwa wa upasuaji, Daharani Juma, amesema kuwa mpaka sasa kambi hiyo imewahudumia wagonjwa takriban 1,500.

Pia alisisitiza umuhimu wa wananchi kujenga utamaduni wa kutambua afya zao mapema ili kuepuka hatari zinazohusiana na magonjwa ya ndani.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *