Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani limefanikiwa kuwafungia leseni madereva 11 wa mabasi ya abiria kufuatia ukiukwaji wa sheria za barabarani, katika operesheni ya kitaifa ya kukagua magari na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali inayoendelea nchini.

Hayo yamebainisha na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, SACP William Mkonda mkoani Geita wakati wa operesheni kama hiyo na kuongeza kuwa, madereva wa maroli makubwa pia wamechukuliwa hatua kali, ambapo baadhi yao wamefungiwa leseni huku wengine wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kukiuka sheria za usalama barabarani.

✍Esther Sumira
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *