Mkurugenzi na mtayarishaji wa gemu maarufu ya ‘Call of Duty’, Vince Zampella (55) amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea California, nchini Marekani.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Jumapili ya Desemba 21, 2025, kwenye barabara kuu ya Angeles Crest Highway baada ya gari aliyokuwa akiendesha aina ya Ferrari kutoka nje ya barabara na kugonga kizuizi kisha kuwaka moto.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa katika gari hiyo, Zampella hakuwa mwenyewe alikuwa na rafiki yake ambaye naye amefariki dunia.

“Kwa sababu zisizojulikana, gari hilo lilitoka nje ya barabara, likagonga kizuizi cha zege, na kumezwa kabisa,” Polisi wa Barabara Kuu ya California walisema katika taarifa na kufichua kuwa gari hilo lililipuka kwa moto.

Zampella ameacha watoto watatu ambao ni Quentin (26), Kyle (22), na Courtney (19), aliyowapata na mkewe wa zamani Brigitte.

Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata katika tasnia hiyo, Zampella alijulikana zaidi kwa kuunda Call of Duty, ambayo imeuza zaidi ya magemu nusu bilioni duniani kote ambayo ina zaidi ya wachezaji milioni 100 wanaocheza kila mwezi.

Baada ya kuanza kama mbunifu wa magemu ya kurusha risasi (shooter games), Zampella alianzisha studio ya Infinity Ward mnamo 2002 na kusaidia kuzindua Call of Duty mnamo 2003.

EA ilithibitisha habari ya kifo cha mkongwe huyo wa magemu duniani, na kuiita hasara isiyoweza kulipwa kwani kazi ya Zampella ilifafanua na kusimulia hadithi za kijeshi hasa kupitia gemu ya Call of Duty.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *