Akizungumza na shirika la habari la Ujerumani DPA, Wadephul alisisitiza kuwa hakutaka kuelezea namna tukio hilo lingetokea, kile anachosisitiza ni Jumuiya ya NATO kuwa tayari kwa vita iwapo vitatokea. Kiongozi huyo amesema kwa sasa Jumuiya hiyo inaongeza uwezo wake wa ulinzi huku Ujerumani nayo ikiimarisha kikosi chake, kuongeza idadi ya wanajeshi pamoja na vifaa vya kivita, ikijipanga kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Amesema Ulaya haipaswi kuridhika iwapo juhudi za kutafuta amani ya Ukraine zitafanikiwa huku akitahadharisha kwamba usalama wa Ulaya, huenda ukatetereka kwa kuitegemea Urusi akiongeza kuwa Moscow, ni lazima iwekwe mbali kabisa ikija katika masuala ya nguvu na Umoja ndani ya Jumuiya hiyo na vikosi vyake vya usalama.

Mwezi uliopita, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius pia alikisema kile alichokisema Wadephul kwamba Urusi huenda ikaishambulia nchi mwanachama wa NATO, upande wa Mashariki mwa Ulaya ifikapo mwaka 2029, baada ya kuimarisha jeshi lake huko. Ujerumani sasa imesisitiza hatua ya kuiunga mkono kikamilifu Ukraine, au kuipa uhakika wa usalama hasa kutoka Marekani wakati mazungumzo au juhudi za kidiplomasia kuhusu usitishaji wa mapigano zikiendelea.

NATO yasema nchi wanachama lazima ziendelee kuiunga mkono Ukraine

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, amezitolea wito nchi washirika wa Ukraine kuendelea kuiunga mkono Kiev, huku akionya kuwa Ulaya itakabiliwa na hatari kubwa za kiusalama ikiwa azma yao itayumba.

Belgien Brüssel 2025 | NATO-Treffen der Außenminister | NATO-Generalsekretär Mark Rutte bei Pressekonferenz
Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte,Picha: Yves Herman/REUTERS

Rutte amesema kwa kuizuwia Urusi kushambulia moja ya nchi za NATO, Ukraine lazima ibakie kuwa imara na kwa kufanya hivyo ni lazima nchi hiyo iungwe mkono kikamilifu na washirika wake wa Ulaya. Amesisitiza umuhimu wa wanachama wa Jumuiya hiyo kuongeza matumizi ya ulinzi kuendana na ahadi zilizokubaliwa katika mkutano wake uliofanyika The Hague mwezi Juni.

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesema Urusi inajitayarisha kufanya mashambulizi nchini humo wakati wa sikuku ya kirismasi. Ameyasema hayo wakati Urusi ikishambulia miundombinu ya nishati mjini Kiev na kusababisha umeme kukatiza katika sehemu kubwa ya mji huo mkuu wa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *