
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza tena mauzo ya nje ya madini ya kobalti, baada ya kusimamishwa kwa kipindi cha miezi 10 ili kupunguza kushuka kwa bei kutokana na usambazaji wa kupita kiasi duniani, serikali ya Kongo imeyasema hayo hii leo.
DRC ndiyo mzalishaji mkubwa wa kobalti duniani ambayo ni madini muhimu kwa betri zinazotumika kwenye magari ya umeme na kwenye simu.
Madini hayo muhimu yanazilishwa zaidi katika eneo la Katanga lililopo kusini mashariki mwa Kongo.
Hata hivyo, licha ya utajiri wake wa madini, Kongo inasalia kuwa miongoni mwa nchi zenye maendeleo duni kabisa duniani kutokana na migogoro, ufisadi, magendo na usimamizi mbaya.