
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz leo Jumanne ameapa kwamba Israeli itaendelea kubaki katika Ukanda wa Gaza na kuahidi kwamba wanapanga kukita kambi zaidi kwa kuanzisha vituo vya ulinzi kaskazini mwa eneo hilo la Palestina.
Katz ameyasema hayo katika hotuba ya video iliyorushwa na vyombo vya habari vya Israeli mapema hii leo.
Katz “tumekita mizizi ndani ya Gaza, na hatutaondoka Gaza kamwe. Tuko pale kulinda, kuzuia yaliyotokea. Kama tulivyosema, tunasimama, tunaamini kwenye maslahi ya Israel na jeshi letu la IDF katika kuilinda Israeli, katika vita vikali kati ya maadui kijihadi wa aina hii, na maadui wa Israeli wa aina hii.”
Hata hivyo, matamshi hayo yamekosolewa vikali na waziri wa zamani,Gadi Eisenkot, ambaye amesema hatua hizo zinaenda kinyume na maslahi ya kitaifa na yanatishia usalama wa Israel katika ukanda huo.