Viongozi wa Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES), kundi linalojumuisha Mali, Burkina Faso na Niger, umeanzisha shirika jipya la habari lenye makao yake makuu mji wa Mali, Bamako.

Televisheni ya AES inasemekana kuwa hatua muhimu katika malengo ya kutoa taarifa huru kwa kundi hilo la Afrika Magharibi, na limeelezwa kuwa chombo rasmi cha kukabiliana na upotoshaji wa taarifa na kuimarisha simulizi ya kanda hiyo.

Ilizinduliwa siku ya Jumanne na Rais wa Mali Jenerali Assimi Goita, Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore na Rais wa Niger Jenerali Abdourahamane Tiani waliokutana mjini Bamako kwa mkutano wa siku mbili kutathmini mwaka mmoja wa muungano wa AES.

Mali, Burkina Faso na Niger walijiondoa rasmi kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) Januari 2025 kufuatia mchakato wa mwaka mzima.

Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Burkina Faso inasema kuwa viongozi hao watatathmini ripoti ya utekelezaji, kufanya maamuzi ili kuangazia mafanikio na kushughulikia changamoto kubwa zinazokabili AES.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *