Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne lilipitisha hatua ya kuongezea mamlaka kwa kikosi kinachoongozwa na Umoja wa Afrika nchini Somalia hadi mwaka 2026.

Tume ya Umoja wa Afrika ya kulinda amani Somalia (AUSSOM) imewekwa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ili kuunga mkono vikosi vya usalama vya Somalia na kupambana na magaidi wa Al Shabab.

Ilibadilisha misheni ya “mpito” iliyokuwepo mwezi Januari, ambayo yenyewe ilikuwa mabadiliko ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichoanzishwa mwanzoni mwa mwaka 2007.

Mwezi Agosti, vikosi vya jeshi la Somalia pamoja na AUSSOM vilikomboa mji wa kimkakati wa Bariire, ulio na kambi ya kijeshi na uko takriban kilomita 100 magharibi ya mji mkuu Mogadishu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *