#HABARI: Waziri mkuu wa Libya amesema, mkuu wa jeshi la Libya amefariki katika ajali ya ndege nchini Uturuki.
Jenerali Mohammed Ali Ahmed al-Haddad na wengine wanne walikuwa ndani ya ndege aina ya Falcon 50 iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Uturuki, Ankara, Jumanne jioni.
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya alisema mawasiliano na ndege hiyo ya biashara yalipotea saa 20:52 saa za eneo (17:52 GMT) – takriban dakika 42 baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Ankara.
Ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Tripoli ilikuwa imetoa ombi la kutua kwa dharura kabla ya mawasiliano kupotea.
Mabaki ya ndege hiyo baadaye yalipatikana Kusini-Magharibi mwa Ankara, na uchunguzi sasa unaendelea kuhusu kilichosababisha ajali hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.