Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, imetoa shilingi Milioni 112.7 zinazotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani, kwaajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu huku wanufaika
wakitakiwa kutumia mipoko hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mwanamwaya Kombo amesema mikopo hiyo ni miongoni mwa mambo ya msingi yatakayotekelezwa na Serikali lengo nikuwanua wajasiriamali hususani Vijana, hivyo wanufaika wote watumie mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Rashid Gembe amevitaka vikundi hivyo kuhakikisha vinarejesha Mikopo hiyo kwa wakati, huku Afisa Maendeleo wa Wilaya hiyo Elizabeth Malali akisema zaidi ya milioni miatano zimetolewa kwa vikundi mbalimbali katika awamu mbili.
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *