Inspector Haroun aachia nyimbo mpya mbiliInspector Haroun aachia nyimbo mpya mbili

MSANII mkongwe wa Bongo Fleva, Haroun Rashidi maarufu kama Inspector Haroun Babu, ameendelea kudhihirisha uimara na ubobezi wake katika muziki baada ya kuachia nyimbo mbili mpya zinazojulikana kama “AI” na “Maisha Ndo Haya Haya.”

Akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam, Inspector Haroun Babu alisema wimbo wa “AI” ameutoa kwa mfumo wa audio pekee, huku “Maisha Ndo Haya Haya” akiuachia kwa audio na video. Amesema ujumbe uliobebwa katika wimbo “Maisha Ndo Haya Haya” unalenga kuhamasisha jamii kutokata tamaa na kutoathiriwa na msongo wa mawazo katika maisha ya kila siku.

Aidha, msanii huyo amebainisha kuwa kazi zote mpya alizozitoa ndani ya kipindi cha wiki mbili zilizopita hazina ushirikiano wa msanii mwingine, kwani amezifanya mwenyewe kuanzia mwanzo hadi mwisho. “Kazi nilizoachia wiki hizi mbili sijamshirikisha mtu yeyote, nimefanya mimi kama mimi,” amesema Inspector Haroun Babu.

Kwa upande mwingine, amefafanua kuwa video ya “AI” ipo katika hatua za maandalizi, ambapo imebuniwa kuwa tofauti kwa kuhusisha teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) kwa kiwango kikubwa. Kwa kuachia kazi hizo mpya, Inspector Haroun Babu amesema bado ana hamu, nguvu na ubunifu wa kuendelea kufanya muziki, akiamini kuwa bado ana mengi ya kuwapatia mashabiki wake. SOMA: Tamasha nyimbo za dini kubadili vijana kimaadili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *