ARUSHA: NAIBU Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi amekiagiza Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC ) kuendeleza bunifu zitakazowezesha kilimo kuwa na mvuto wakati serikali ikiendelea kusukuma nguvu katika mpango wa bajeti 2026/27.

Katambi ametoa agizo hilo jijini Arusha wakati alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho na kujionea zana mbalimbali za kilimo yanayowasaidia wakulima maeneo mbalimbali nchini kujikwamua kiuchumi na kuona kuwa kilimo ni ajira.

Amesisitiza kituo hicho kuendelea kuweka vituo mbalimbali vya matumizi ya zana za kilimo ili kujua mahitaji ya wakulima ikiwemo mfumo rahisi wa ukodishaji kwa wakulima haswa katika mazao ya na mahindi, ufuta, dengu na nk.

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Camartec, Mhandisi Godfrey Mwinama ametaja baadhi ya changamoto kuwa ni kukosekana kwa maabara sahihi za kufanya majaribii ya zana za kilimo na teknolojia vijijini, kukosekana kwa karakana za uzalishaji, uchakavu wa mashine za karakana ni baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *