Steinmeier, amebainisha kuwa wengi wanafuatilia juhudi zilizoongezeka za kidiplomasia za kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine kwa matumaini, lakini pia kwa mashaka na wasiwasi.
Ameongeza kusema Ulaya inapaswa kutambua kwa pamoja nguvu na maadili yao ili kuchukua hatua.
Rais huyo, ambaye muhula wake unamalizika mwaka 2027, pia amewataka Wajerumani kuwa na ujasiri na kukumbatia mabadiliko.
