#HABARI: Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Boniface Jacob, amesema kuwa katika suala la kutafuta maridhiano ya kisiasa nchini, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba ni mojawapo kati ya watu wanaoweza kuaminiwa kusimamia au kuwa sehemu ya mchakato huo.

Boniface ameeleza kwamba Mzee Warioba ameonesha jitihada za wazi hata kabla ya uchaguzi za kutaka kuliweka taifa pamoja, na hivyo anaweza kuaminiwa kushiriki katika kutafuta suluhu ya mgawanyiko wa kisiasa kwa pande zinazotofautiana.

“Mfano tukiwa bado hatujaenda kwenye uchaguzi tukiwa na mivutano ya ‘no election’ na wengine wakisema Oktoba tunatiki nchi nzima nilimuona Mzee mmoja tu aliyefanya jitihada kwanza aliwatafuta tume ya uchaguzi kwa kuwabembeleza kwamba ikiwezekana uchaguzi usifanyike ili haya makundi mawili yakubaliane kwanza”

“Nilimsikia akisema kwamba pamoja na jitihada hizo tume walimkatalia kuonana nae wakamjibu kwamba kama ana jambo aandike barua, kwa kujinyenyekeza pamoja na kwamba ni mtu mkubwa Mzee mstaafu wa nchi hii akaandika barua kuwajulisha tume mtazamo wake”

“Kwamba anatamani makundi yanayosigana yakubaliane kwanza kabla ya uchaguzi ambaye Mzee huyo ni Jaji Warioba pamoja na kwamba hakufanikiwa lakini alionesha kwamba amejali”

“Mtu wa namna hiyo ukimuweka kwenye tume tayari ameonesha kujali tangu mwanzo kwahiyo angejitokeza watu wangekuwa na imani kwamba yule Mzee angeweza kuwa ni mwaminifu”-Boniface Jacob.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *