Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ametoa siku kumi kwa Msimamizi wa Miradi ya Serikali (TECU) Mkoa wa Songwe kuwasilisha mpango kazi unaoonesha lini ujenzi wa barabara ya Isongole utakamilika.
Agizo hilo limetolewa baada ya kukagua mradi wa kilometa 52 unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 74 na kubaini kusuasua kwa utekelezaji wake.
Kwa mujibu wa TANROADS, mradi ulioanza Desemba 2024 ulipaswa kufikia asilimia 40 ndani ya mwaka mmoja, lakini hadi sasa umefikia asilimia 8 pekee, hali iliyomfanya Naibu Waziri kueleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi.
Mhariri| @claud_jm
#AzamTVUpdates