
Mchezo huu uliopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca ulikuwa na ushindani mkubwa, huku Guinea ya Ikweta wakionyesha upinzani mkali lakini walishindwa kuidhibiti Burkina Faso na dakika za majeruhi ndizo zilizoamua hatma ya pambano.
Guinea ya Ikweta walitangulia kufunga, licha ya mchezaji wao Basilio Ndong kurambishwa kadi nyekundu dakika ya 50 ya mchezo. Bao lilipatikiana dakika ya 85 kupitia Marvin Anieboh.
Burkina Faso walipata bao la kusawazisha muda ziada dakika ya 95 kupitia Georgi Minoungou, na dakika tatu baadaye, mashabiki wa The Stallions walisherehekea bao la ushindi kutoka kwa Edmond Tapsoba.
Burkina Faso sasa wanaanza kampeni yao ya AFCON kwa alama tatu muhimu, huku kundi lao likionekana kuwa na ushindani mkali.
Kwa sasa, Burkina Faso wanaongoza kundi lao, na mashabiki wao wana matumaini makubwa kuelekea mechi zinazofuata.