Msemaji wake ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, amenukuliwa na shirika la habari la Interfax, kwamba Rais Vladimir Putin amepewa taarifa kuhusu mazungumzo hayo na kwamba Moscow inaendelea kuandaa msimamo wake huku ikiwasiliana na maafisa wa Marekani.

Mpango huo unajumuisha mapendekezo ya dhamana za usalama kutoka Magharibi kwa Ukraine zinazofanana na kifungu cha ulinzi wa pamoja cha jumuiya ya NATO, huku ukipendekeza ukubwa wa jeshi la Ukraine uwe wanajeshi 800,000.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwaambia waandishi wa habari kuwa ingawa Kiev, Marekani na Ulaya wamekubaliana juu ya masuala kadhaa makubwa, suala kuu linalozuia makubaliano ni udhibiti wa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *