
Mkuu wa Umoja wa Ulaya Antonio Costa amelaani vikali marufuku ya kuingia Marekani iliyowekwa, akisisitiza kuwa haikubaliki kati ya washirika, wadau na marafiki na ameiomba Marekani kutoa ufafanuzi.
Katika taarifa yake,Tume hiyo imesema ililazimika itachukua hatua za haraka na madhubuti kulinda uhuru wa kisheria dhidi ya hatua zisizo na msingi.
Hata hivyo haikuwekwa wazi ni hatua gani inaweza kuchukua endapo mzozo huo utazidi kuongezeka. Huenda inaweza kupendekeza kupunguza ushirikiano na Marekani katika maeneo fulani, au hata kuchukua hatua za kiuchumi.