
Takriban wakimbizi nane kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongowaliokimbilia nchini Burundi wamekufa kwa ugonjwa wa kipindupindu, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi katika shirika la misaada linalowahudimia wakimbizi hao.
Mfanyakazi huyo ameonya kwamba maelfu ya watu wanakabiliwa na hali mbaya na ya kutisha baada ya kukimbilia Burundi kufuatia hatua za hivi punde ya kundi la waasi waM23katika mji wa Uvira mashariki mwa DRC.
Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ni kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya M23 yamesababisha wakimbizi wa ndani kufikia 500,000 katika jimbo laKivu Kusini pekee nchini Kongo, wakiwemo 200,000 ndani ya eneo la Uvira.
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa ufadhili wa haraka wa dola milioni 33 ili kuweza kuwasaidia wakimbizi hao.