
Wataalam waUmoja wa Mataifa wamesema leo katika ripoti maalum kwamba kundi la wanamgambo lenye itikadi kali la Al-Shabab linasalia kuwa tishio kubwa zaidi la kiusalama nchini Somalia na nchi zinazoizunguka nchi hiyo hasa Kenya.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa licha ya juhudi zinazoendelea za vikosi vya Somalia na kimataifa katika kuzuia operesheni za kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaida, bado uwezo wa kundi hilo haujapungua.
Mapema wiki hii, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja kukiongezea muda kikosi cha Umoja wa Afrika cha “kuunga mkono na kuleta utulivu” nchini Somaliahadi Desemba 31, 2026. Kikosi hicho kinajumuisha walinda amani 11,826.
Ripoti hiyo inakadiria kwamba mwaka huu, Al-Shabab walifanya wastani wa mashambulizi sita kwa mwezi nchini Kenya, hasa katika kaunti za Mandera na Lamu ambazo zinapakana na Somalia.