Muungano wa Mieleka Duniani (UWW) umemtaja Rahman Amouzad kutoka Iran kuwa mwanamieleka wa mtindo wa freestyle (kujiachia) “Aliyeng’ara Zaidi” kwa mwaka huu 2025.

“Amouzad alikuwa mkamilifu ulivyoweza kuwa katika msimu, akirejea kwenye umaarufu kwa juhudi za kushinda taji kwenye Mashindano ya Dunia, Michezo ya Mshikamano wa Kiislamu na Mashindano ya Muhamet Malo Ranking Series, na kumaliza msimu kama mwanamieleka aliyeorodheshwa nambari 1 duniani.

UWW imetangaza kwenye taarifa iliyotumalijinyakulia pointi 58,000 kwenye uorodheshaji wa kimataifa wa Ranking Series, huku akichota “rekodi isiyo na dosari ya alama 14-0” kwa mwaka huu 2025.

Shirikisho hilo la mieleka duniani limeeleza kuwa, Ushindi mara tano kati ya mapambano yake yote mwaka huu ulikuwa dhidi ya “wapinzani wa ngazi ya juu” wanaoshikilia medali za dunia au Olimpiki, wakiwemo Real Woods kutoka Marekani, Umidjon Jalalov kutoka Uzbekistan, Taiyrbek Zhumashbek Uulu, raia wa Kyrgyzstan, na Mjapani Kotaro Kiyooka.

“Cha kustaajabisha zaidi kuhusu mechi hizo tano dhidi ya mabingwa wa dunia, Amouzad alishinda alama 42-4,” UWW imesema, na kuongeza kuwa, “kivutio hicho kikuu cha msimu kwa Amouzad” kilikuja katika Mashindano ya Dunia ya Mieleka ya 2025 huko Zagreb. Amouzad, “ana umri wa miaka 23 pekee na bado anaendelea kuwa bora zaidi,” UWW imebainisha.

Aidha mapema wiki hii, Saeed Esmaeili wa Iran alitawazwa kuwa mwanamieleka “Aliyetawala Zaidi” wa mwaka huu 2025, katika mieleka mtindo wa Greco-Roman.

Timu ya taifa ya mieleka ya kujiachia (freestyle) ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara kadhaa imetwaa ubingwa wa mashindano ya dunia ya mchezo huo. Aidha timu dada ya mieleka ya Greco-Roman ya Iran imekuwa ikifanya vizuri pia na kuipaisha Jamhuri ya Kiislamu katika mapambano ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *