Mlipuko ulitokea katika msikiti wakati wa sala za jioni Jumatano katika eneo la Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno nchini Nigeria, kwa mujibu wa shududa.
Kulingana na vyanzo, shirika la habari la AFP linaripoti kwamba takriban watu saba waliuawa katika mlipuko.
Jimbo la Borno limekumbwa na mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara, yakiuwa maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni kuachana na makazi yao kaskazini-mashariki.