Dunia inaadhimisha sikukuu ya Krismasi Alhamisi Desemba 25, siku ambayo Wakiristo wanakumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo, ambapo ibada zinafanyika Makanisani, huku wengine wakisherehekea majumbani na katika maeneo mengine ya starehe.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika huku baadhi ya mataifa kama Sudan na Ukraine yakiendelea kukabiliwa na vita.
Kwa mara ya kwanza, sikiuuu ya Krismasi inaadhimishwa kwenye mji wa Bethlhem, uliopo kwenye mamlaka ya Palestina, inakoaminiwa alizaliwa Yesu Kristo.
Sherehe za mwaka huu zinafanyika baada ya kupatikana kwa mkataba wa kusitisha vita kati ya kundi la Hamas na Israel miezi kadhaa iliyopita.
Katika mkesha wa wa Krismasi siku ya Jumatano, mamia ya wauamini wa Kikiristo walifurika katika Kanisa kuu mji wa Bethlehem, kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Mjini Vatican, kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Leo wa Kumi na sita, anaongoza misa ya Krismasi yake ya kwanza baada ya kushika nafasi hiyo.
Katika ujumbe wake wakati wa mkesha wa sikukuu hii, kiongozi huyo ametoa wito wa kuwepo kwa amani kote duniani, hasa katika saa 24 za maadhimisho ya Krismasi.