Mataifa ya Ulaya  sambamba na Canada na Japan yametoa taarifa ya pamoja na kulaani uamuzi wa Israel wa kuanzisha ujenzi mpya wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Taarifa hiyo ya pamoja imetiwa saini na nchi 12 za Ulaya, zikiwemo Ubelgiji, Ufaransa, Uingereza, na Ujerumani; pamoja na Canada na Japan. Mataifa hayo yameonya kwamba, hatua kama hizo zinakiuka sheria za kimataifa na zinaweza kushadidisha ukosefu wa utulivu wa kikanda.

Mataifa hayo yamebainisha “upinzani wao wa wazi” kwa aina yoyote ya unyakuzi wa ardhi ya Palestina na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, ikiwa ni pamoja na idhini ya makazi ya E1 na maelfu ya vitogoji vipya vya walowezi.

Taarifa hiyo imesisitiza juu ya haki ya Wapalestina ya kujiainishia mustakabali wao na kuundwa nchi huru ya Palestina. Umoja wa Mataifa umetangaza mara chungu nzima kwamba, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na utawala wa Israel katika maeneo ya Wapalestina ni kinyume cha sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *