Diddy aomba rufaa kupinga kifungo chake gerezaniDiddy aomba rufaa kupinga kifungo chake gerezani

MSANII maarufu wa muziki wa rap, Sean “Diddy” Combs, ameomba Mahakama ya Rufaa ya Marekani imwachilie huru na kutengua hukumu yake ya kifungo cha miezi 50 gerezani alichohukumiwa kutokana na makosa mawili yanayohusishwa na ukahaba.

Ombi hilo limewasilishwa katika Mahakama ya Rufaa ya Jimbo la Pili, New York, ambapo timu ya mawakili wake imeeleza kuwa hukumu hiyo haikufuata misingi sahihi ya sheria. SOMA: Sean ‘Diddy’ Combs kuhukumiwa Oktoba 3

Wakili Alexandra Shapiro amesema mahakamani kuwa hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikosea kwa kutegemea ushahidi uliohusishwa na mashtaka ambayo yalionekana kutokuwa sahihi, hivyo kufanya hukumu hiyo kuwa “isiyo halali, kinyume cha katiba na inayopotosha haki za msingi za mtuhumiwa”.

Aidha, kupitia ombi hilo, mawakili wake wameiomba mahakama hiyo kubatilisha kabisa hukumu hiyo au kuamuru kesi hiyo ianze upya na endapo ombi hilo halitawezekana, wanaomba kifungo chake kipunguzwe.

Combs mwenye umri wa miaka 56 kwa sasa anatumikia kifungo cha zaidi ya miaka minne gerezani katika jimbo la New Jersey, kufuatia kutiwa hatiani chini ya sheria ya “Mann Act” inayohusiana na usafirishaji wa watu kwa madhumuni ya ukahaba. Wakili Shapiro pia ameomba mchakato wa rufaa uharakishwe ili kumwezesha Combs kunufaika endapo rufaa yake itasikilizwa na kuamuliwa mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *