Chanzo cha picha, SAUL LOEB/POOL/EPA-EFE/REX/Shutterstoc
Muda wa kusoma: Dakika 5
1. Uapisho wa Donald Trump
Donald Trump alirejea tena katika Ikulu ya White House baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa 47 wa taifa hilo Jumatatu tarehe 20 Januari 2025.
Trump alianza kazi akiahidi “enzi mpya” kwa nchi hiyo na kutangaza hatua kama vile “dharura ya kitaifa” kwenye mpaka na Mexico na kuwarudisha mamilioni ya wahamiaji.
Rais alirudia kauli ya kutishia kurejesha udhibiti wa Mfereji wa Panama katika Amerika ya Kati, na kutangaza kwamba atabadilisha jina la Ghuba ya Mexico kuwa Ghuba ya Marekani “Gulf of America” – ingawa haikujulikana jinsi hilo litakavyofanyika.
Rais alitumia sehemu ya kwanza ya hotuba yake kuahidi “taifa ambalo ni la kujivunia, lenye mafanikio na huru.”
“Uhuru wetu utarejeshwa, usalama wetu utarejeshwa, uzito wa haki utarejeshwa tena,” Trump alisema.
Trump baadaye alitangaza mfululizo wa hatua na vipaumbele. zaidi soma hapo chini.
2. Ushuru wa Trump Kimataifa
Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2025 ulishuhudia Rais wa Marekani, Donald Trump, akitangaza viwango vipya vya ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo, viwango ambavyo havijaonekana tangu mwanzoni mwa karne iliyopita.
“Leo ni Siku ya Ukombozi,” Trump alisema . “Ni moja ya siku muhimu katika historia ya Marekani, na ni tangazo la uhuru wa kiuchumi wa Marekani.”
“Tutaifanya Marekani kuwa kubwa na tajiri tena. Nchi yetu imenyang’anywa kwa zaidi ya miaka 50. Hilo halitafanyika tena.” alisema mwanzaoni mwa 2025 alipotangaza hatua hiyo iliyotikisa ulimwengu wa biashara mara baada ya kiongozi huyo kurejea Ikulu ya White House.
Kwa ujumla, hakuna nchi iliyoepuka ushuru wa Wamarekani kwa ununuzi wa bidhaa zao ambapo “kiwango cha chini cha ushuru” kitakuwa 10%.
Februari 4: 10% ushuru kwa bidhaa kutoka China
Machi 4: 10% ya ushuru kwa bidhaa za China iliongezeka mara mbili hadi 20%
Machi 5: Msamaha wa ushuru kwa mwezi mzima kwa magari yanayotengenezwa Amerika Kaskazini ambayo yanatii makubaliano ya biashara huria.
Machi 6: Msamaha wa ushuru kwa bidhaa zinazotoka katika chini zenye makubaliano ya biashara huria za Amerika Kaskazini, kama vile televisheni, viyoyozi, maparachichi na nyama ya ng’ombe.
Ushuru wa kemikali ya potashi – inayotumiwa katika mbolea na wakulima wa Marekani – ilipunguzwa kutoka 25% hadi 10%
magari vinavyoagizwa kutoka nje kuanzia mwezi wa Mei.
Machi 12: 25% ya ushuru kwa bidhaa zote za chuma na alumini
Aprili 2: Ushuru wa 25% kwa magari yanayoingia Marekani. Ushuru wa 25% kwa vipuri vya magari vinavyoagizwa kutoka nje kuanzia mwezi wa Mei.
Pata maelezo zaidi kuhusiana na ushuru mpya wa Trump alioutangaza mwanzoni mwa kmwaka 2025.
3. Papa Leo XIV na ukurasa mpya wa Kanisa Katoliki
Chanzo cha picha, Reuters
Kardinali Robert Francis Prevost aliandikisha historia mpya mwaka 2025 ndani ya Kanisa Katoliki baada ya kuchaguliwa kuwa Papa wa 267 kuongoza kanisa hilo lenye watu bilioni 1.4 duniani.
Prevost alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Papa Francis, katika kongamano la siku mbili lililofanyika katika Jiji la Vatican.
Papa huyu wa kwanza kutoka Marekani, ni kiongozi anayetajwa kuwa na mwelekeo wa kuendeleza mageuzi ya hayati Papa Francis, huku akisisitiza huduma kwa maskini na makundi maalum katika jamii.
Papa Leo alisimikwa rasmi katika Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja wa St Peter’s Square mnamo tarehe 18 Mei. Soma zaidi:
4. Vita vya Israel na Hamas
Chanzo cha picha, Reuters
Je, ni kwa namna gani kundi ambalo limetawala Ukanda wa Gaza kwa takriban miaka 20, likiowangoza Wapalestina milioni mbili kwa mkono wa chuma na kupigana na Israel mara kwa mara, ghafla linaweka chini silaha zake na kuachia madaraka?
Hili ni swali ambalo limetawala vichwa vya habari mwaka 2025 tangu mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi hilo la Kipalestina yalipoanza.
Mahasimu hao wawili wamekuwa wakikabana koo katika nipe nikupe iliyowahangaisha wapatanishi wa mzozo huo mjini Doha Qatar.
Tangu mpango wa amani wa Gaza uliosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuanza kutekelezwa bado pande hizo mbili zimekuwa zikilaumiana kukiuka makubaliano.
Kwa kuzingatia mtiririko wa picha za kutisha zinazoibuka kutoka Gaza tangu usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa tarehe 10 Oktoba, Hamas inaonekana kuwa na nia ya kurejesha mamlaka yake.
Wapiganaji wake waliofunika nyuso wamerejea mitaani, wamekuwa wakionekana wakiwapiga na kuwaua wapinzani.
Waathiriwa wengine, wale wanaoonyesha uoga, wanapigwa risasi za miguuni kupigwa kwa marungu. Bonyeza hapo chini kwa maelezo na uchambuzi zaidi:
5.Vita vya Urusi na Ukraine

Mwaka 2025 unaelekea kufikia kikomo bila kupatikana kwa ufumbuzi wa mzozo wa Urusi na Ukraine. Juhudi kadha wa kadha zimefanywa na Marekani kumaliza mzozo huo lakini bado hali imesalia kuwa ya ati ati.
Katika wiki za mwanzo za muhula wa pili wa urais wa Trump, Moscow na Washington zilionekana kuanzisha upya uhusiano wao wa nchi mbili.
Wakati fulani ilionekana kana kwamba Vladimir Putin na Donald Trump walikuwa kwenye njia moja, wakielekea upande uleule.
Mwezi Februari Marekani iliegemea upande wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, kwa kupinga azimio lililoandaliwa na Ulaya la kulaani “uvamizi” wa Urusi nchini Ukraine.
Rais wa Marekani, Donald Trump aliharakisha juhudi za kuishinikiza Moscow kukomesha mapigano: kwa kutangaza makataa, matakwa, vitisho vya vikwazo vya ziada dhidi ya Urusi na ushuru mkubwa kwa washirika wa kibiashara wa Urusi, kama India na China.
Kwa upande wake Rais wa Urusi, Vladimir Putin licha ya yote hayo hajaonyesha nia ya kutaka kumaliza mapigano wala kutangaza kusitisha vita hivyo vya muda mrefu. Zaidi soma hapo chini.