#MICHEZO: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema Tanzania inatumia fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), katika kujitangaza na kukaribisha wadau na wawekezaji katika sekta ya utalii ili kutanua wigo wa utalii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Rabat, Morocco Mhe. Chande amesema kuwa jambo kubwa linalowavutia wawekezaji wengi kuwekeza katika sekta ya utalii nchini Tanzania ni kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii vilivyoibuliwa na kutangazwa vyema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya “Tanzania: Royal Tour”.

Adha, amesema kupitia michuano hiyo inayoendelea nchini humo, serikali kupita wizara hiyo imejifunza vya kutosha uwekezaji mkubwa wa miundombunu bora, ya kisasa na kuvutia iliyofanywa na taifa hilo jambo ambalo limesaidia kupokea watalii wengi kila mwaka

“Kwa Afrika, Morocco ni miongoni mwa nchi inayoongoza kuingiza watalii wengi kila mwaka, tunatamani kuwafikia na tumeshaona baadhi ya miundombinu wanayoitumia, na sisi tunakwenda kuiboresha ya kwetu, ili kusudi tufikie idadi tuliyoelekezwa ya kufikia watalii Milion 8 ifikapo 2030, hilo linawezekana, kupitia hii AFCON tu.” Mhe. Chande amesisitiza.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *