Katika eneo la Odessa la kusini-magharibi mwa Ukraine, shambulio la droni la Urusi limesababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wawili, pamoja na kuharibu miundombinu ya bandari na nishati.
Wizara ya Nishati ya Ukraine imesema mashambulizi hayo yamesababisha kukatika kwa umeme katika maeneo mengi hali ambayo viongozi wa Ukraine wameitaja kuwa hatari zaidi wakati wa majira ya baridi na kuishutumu Moscow kwa ugaidi wakati huu wa Krismasi.
Urusi, ambayo husherehekea Krismasi kwa mujibu wa imani ya kanisa la Orthodox, hapo Januari 7, imekataa wito wa kusitisha mapigano kipindi cha sikukuu. Wakati huo huo, mashambulizi ya droni ya Ukraine yamesababisha moto mkubwa kwenye matenki ya kuhifadhi mafuta katika mji wa bandari wa Temryuk kusini mwa Urusi. Ukraine imekuwa ikipambana na uvamizi kamili wa Urusi tangu Februari 2022.
